Joy FM

Kigoma imeanza kutumia e-Ardhi kuimarisha huduma za ardhi

14 September 2026, 12:35

Kamishana wa ardhi kutoka Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Makwasa Biswalo, Picha na Josephine Kiravu

Matumizi ya teknolojia yanavyoweza kuongeza kasi ya utoaji wa huduma za ardhi.

Na Josephine Kiravu

Mkoa wa Kigoma umeanza rasmi kutumia mfumo wa Kielektroniki wa E ardhi, hatua inayotajwa kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za ardhi kwa wananchi.

Akizungumza na wanahabari mkoani Kigoma Kamishana wa ardhi kutoka Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Makwasa Biswalo,amesema matumizi ya mfumo huo tayari yameongeza ufanisi katika utendaji kazi huku yakipunguza muda wa kushughulikia huduma za ardhi.

Sauti ya Kamishna ardhi
Kamishana wa ardhi kutoka Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Makwasa Biswalo, Picha na Josephine Kiravu

Kwa upande wake, Afisa ardhi mkuu wizara ya ardhi Hisani Mtolera pamoja na Kamishna wa ardhi mkoa wa Kigoma Tumaini Gwakisa wamesema mwitikio wa wananchi katika kutumia mfumo huo ni mzuri kwani mpaka sasa wananchi wanaendelea kujiandikisha na kutumia mfumo huo mpya.

Sauti ya Gwakisa na Mtolera
Afisa ardhi mkuu wizara ya ardhi Hisani Mtolera, Picha na Josephine Kiravu

Kwa mujibu wa kamishna wa ardhi hatua hiyo ya kutumia mfumo huo wa kielektroniki wa E ardhi inaonesha namna matumiz ya teknolojia yanavyoweza kuongeza kasi ya utoaji wa huduma za ardhi na kupunguza changamoro zilizokuwa zikijitokeza katika taratibu za awali.