Joy FM

Idara ya mazingira Kigoma MC yatakiwa kuondoa taka kwa wakati

22 April 2026, 15:46

Mkuu wa Wilaya Kigoma Rashid Chuachua akiwa katika kikao cha kamati ya siasa ya CCM, Picha na Emmanuel Matinde

Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imeanza kutekeleza zoezi la uondaaji wa taka zilipo katika vizimba ikiwa ni mkakati wa kufanya mji wa Kigoma kuwa msafi

Na Mwandishi wetu

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kigoma Mjini imeilekeza idara ya mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, kuboresha hali ya usafi kwa kuondoa taka ambazo zimekuwa zikizagaa ovyo katika baadhi ya maeneo.

Hatua hiyo ni baada ya wajumbe wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kigoma kueleza kuwa hali ya usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji hairidhishi ikiwemo maeneo yaliyowekwa vizimba kwa ajili yaa kukusanyia uchafu.

Sauti ya Sauti Mjumbe
Wanachama na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya Kigoma Mjini wakiwa kwenye kikao, Picha na Emmanuel Matinde

Awali akijibu hoja za wajumbe wa kikao hicho Afisa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji, ameelezza baadhi ya mikakati iliyopo ya kuondoa taka zinazozagaa ili kuweka mazingira ya mji katika hali ya usafi.

Sauti ya Afisa Mazingira

Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini Sadick Kadulo aliyeongoza kikao hicho kwa niaba ya Mwenyekiti Ahmed Mwilima, ameitka idara hyo kuongeza bidii ya usafi wa mazingira hasa katika maeneo yaliyokithiri kwa uchafu.

Sauti ya Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini