Joy FM
Joy FM
15 June 2026, 17:02

Serikali imeendelea kuwezesha vikundi mbalimbali vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mikopo inayotolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani ili viweze kufanya shughuli za uzalishaji mali
Na Sadick Kibwana
Serikali Mkoani Kigoma imetoa zaidi ya shilingi bilioni mbili nukta moja kwa vikundi 340 vya uzalishaji mali mkoani Kigoma kwa lengo la kuwainua wananchi kiuchumi.
Akizungumza kwenye kongamano la fursa za kiuchumi, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu, amewataka wananchi kutuma vyema fursa zilizopo ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.
Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Mji Kasulu, Bi. Catherine Mchilo ameeleza namna makundi husika yanavyoweza kuzifikia na kuzitumia fursa hizo za kiuchumi.
Aidha, Bi. Catherine amebainisha taratibu za upatikanaji wa mikopo hiyo na namna ya kurejesha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Soko la Sofya Pearl Rafael, ameeleza kuwa hawajafanikiwa kupata mkopo licha ya kufuata taratibu zote zilizowekwa.
Mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri za Mitaa imekusudiwa kwaajili ya kuwainua kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambapo hawako kwenye mfumo wa rasmi wa ajira.