Joy FM

Dkt. Nchimbi kufanya ziara ya kampeni Kigoma

10 October 2025, 08:05

Mgombea Mwenza wa Rais Samia Suluhu Hassan, Dkt. Balozi Emmanuel Nchimbi, Picha na CCM Tanzania

Mgombea Mwenza wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kinyang’anyiro cha Urais wa Tanzania katika mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt.Balozi Emmanuel John Nchimbi anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya kampeni Mkoani Kigoma kuanzia Kigoma Oktoba 12 na 13.

Katibu wa siasa, uenezi na mafunzo wa CCM Mkoa wa Kigoma Deogratius Nsokolo amesema Dkt. Nchimbi atapokelewa na wanaccm na wananchi katika uwanja wa ndege wa kigoma jumapili asubuhi oktoba 12 ambapo baada ya kusalimiana na wananchi wa kigoma mjini ataelekea wilaya ya Kakonko ambako atakuwa na mkutano wa hadhara asubuhi.

Katibu wa siasa, uenezi na mafunzo wa CCM Mkoa wa Kigoma Deogratius Nsokolo, Picha na CCM Kigoma

Katika mkutano huo wa kampeni ambao utafanyika mjini Kakonko Mgombea mwenza wa CCM atautunia kuomba kura kwa wagombea wa CCM, Mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea ubunge katika jimbo la Kakonko Allan Mvano na wagombea udiwani kupitia ccm kutokakata 13.

Mchana Dkt. Emmanuel John Nchimbi atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Taifa mjini Kibondo na kuwanadi na kuwaombea kura wagombea wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge katika jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo Dr. Florence Samizi na wagombea udiwani katila kata 19.

Nsokolo amesema Jumatatu Oktoba 13, Dkt Emmanuel Nchimbi, asubuhi atafanya mkutano mkubwa wa kampeni uwanja wa Kazegunga kata ya Mungonya jimbo la Kigoma kaskazini Wilayani kigoma ambapo pamoja na kumnadi mgombea Urais wa CCM atamnadi mgombea ubunge katika jimbo hilo Peter Joseph Serukamba na wagombea 16 wa udiwani.

Kufuatia ziara hiyo ya kampeni, Nsokolo amewataka wanachama wa CCM na wananchi kujitokeza kwa wingi katika mikutano hiyo ili kusikia Sera,ilani na mipango ya Serikali ijayo ya Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuundeleza Mkoa wa kigoma na Taifa kwa ujumla na kwamba maandalizi yamekamilika.

Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani utafanyika oktoba 29 mwaka huu ambapo ambapo Mkoa wa Kigoma una majimbo nane ya uchaguzi na kata 139.