Joy FM

Wananchi waaswa kujiepusha na mikopo umiza

3 March 2026, 11:14

Meneja msaidizi Idara ya mawasiliano kutoka Benki kuu ya Tanzania BoT Bi. Noves Moses, Picha na Josephine Kiravu

Katika miaka ya karibuni, kumekuwa na ongezeko la taasisi na programu za simu zinazotoa mikopo ya haraka inayojulikana kama mikopo kausha damu na mikopo hii huvutia watu wengi kwa sababu ya urahisi wa kuipata bila dhamana kubwa au taratibu ndefu hata hivyo, nyuma ya urahisi huo kuna madhara makubwa yanayoweza kuathiri mtu binafsi, familia na hata jamii kwa ujumla.

Na Josephine Kiravu

Jamii Mkoani Kigoma imetakiwa kujenga utamaduni wa kukopa na kulipa, ili kuepuka madhara yanayoweza kuwakumba ikiwemo deni walilokopa kuongezeka na kuwafanya kushindwa kukopesheka kwenye taasisi zingine.

Hayo yameelezwa na Meneja msaidizi Idara ya mawasiliano kutoka Benki kuu ya Tanzania BoT Bi. Noves Moses ambapo amessisitiza kukopa na kulipa kwa uaminifu kwani baadhi ya Watanzania bado wapo nyuma.

Meneja msaidizi Idara ya mawasiliano kutoka Benki kuu ya Tanzania BoT Bi. Noves Moses, Picha na Josephine Kiravu
Sauti ya Meneja msaidizi Idara ya mawasiliano kutoka Benki kuu ya Tanzania BoT Bi. Noves Moses,

Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakichukua mikopo mingi bila kuangalia namna gani watalipa au kuangalia biashara zao kama zitawawezesha kulipa na kuwafanya kushindwa kurejesha kwa wakati.

Sauti ya Meneja msaidizi Idara ya mawasiliano kutoka Benki kuu ya Tanzania BoT Bi. Noves Moses,

Bi Fatma Abdalla ni mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye alikopa kiasi cha shilingi milioni mbili na baada ya kushindwa kurejesha kwa wakati riba ilifika kiasi cha shilingi million 2 na elf 50 huku akitishiwa maisha yake na vikundi vilivyomkopesha.

Sauti ya Bi Fatma Abdalla ni mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji

Hata hivyo licha ya changamoto hizo alizopitia mwanamama huyo ikiwemo kukimbiwa na mwenza wake  lakini kwa sasa maisha yake yanaendelea vyema huku akiwashauri wananchi wenzake kutojiingiza kwenye mikopo bila ya kufanya utafiti wa kile unachokusudia kufanya kwani madhara ya ni makubwa hapo baadaye.