Joy FM
Joy FM
24 April 2026, 12:22

Siku chache baada ya Serikali ya Mkoa wa Kigoma kuendesha operesheni ya kuwasaka wahamiaji haramu na wakimbizi waliotoka kwenye kambi na kuingia kuingia kwenyemakazi ya watu ili kuwarusha nchi kwa, Ubalozi mdogo wa Burundi Mkoani Kigoma umetoa neno
Na Timotheo Leonard
Balozi mdogo wa Burundi Mkoani Kigoma, Mhe. Kekenwa Jeremiah, ametoa wito kwa raia wa Burundi wanaokusudia kuingia nchini Tanzania kuhakikisha wanafuata taratibu za kisheria kwa kupata vibali halali kabla ya kuingia na kuisha katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo hiki ofisini kwake, Mhe. Jeremiah amesisitiza umuhimu wa raia wa Burundi kuheshimu sheria za nchi jirani ili kudumisha uhusiano mwema na usalama baina ya Tanzania na Burundi.
Aidha, Mhe. Jeremiah ametoa agizo kwa raia wote wa Burundi ambao tayari wapo nchini Tanzania bila vibali rasmi, kurejea nchini kwao haraka ili kufuata utaratibu unaostahili wa kisheria.
Wito huo unakuja kama sehemu ya jitihada za ubalozi huo kuhakikisha usalama na utaratibu wa kisheria unazingatiwa, huku ukimarisha ushirikiano wa mipakani kati ya Tanzania na Burundi ambapo hivi karibuni serikali ya Mkoa wa Kigoma iliendesha operesheni ya kuwakamata wahamiaji harumu na kuwarudisha nchi Burundi