Joy FM
Joy FM
21 April 2026, 09:45

Usafi wa mazingira umetajwa kuwa nguzo muhimu katika kulinda afya za wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi na wataalamu wa afya wanasema kuwa mazingira safi huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, malaria na kuhara.
Na Emmanuel Kamangu
Wanachama wa chama Cha demkrasia na maendeleo chadema na viongozi chama hicho Wilaya ya Kasulu wamekutana kufanya usafi katika ofisi za Wilaya huku wakihimizana kuwa wamoja katika kuhakikisha chama kinakuwa imara.
Wanachama hao wa chadema wakiongozwa na viongozi wao ngazi ya wilaya ya Kasulu wameonekana kuwa wenye furaha kufuatia mahakama ya rufani kutupilia mbali zuio la mda lililokuwa limewekwa dhidi ya chama chao kutojishugulisha na shuguli za siasa ikiwemo za kiutendaji.
Baadhi ya viongozi wa majimbo mawili kasulu mjini na vijijini wakiwa pamoja na wanachama wao katika zoezi la kusafisha ofisi ya chadema wilaya wamewaomba wanachama wao kuwa wamoja ili kuendelea kukijenga chama kikamilifu kuanzia ngazi ya msingi ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha chama kinaimalika zaidi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kasulu Bw, Fanuel kisabo amesema kuwa licha ya chama hicho kujeruhiwa wakiwemo viongozi wake kupitia magumu ila bado wako ngangari kuhakikisha chama kinaendelea kuwa sauti ya watanzania.
Ikumbukwe chadema kimekuwa korokoroni kwa siku 310 kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa chadema Zanzibar Bw, Said issa Mohamed akishirikiana na wenzake wawili wakidai kuwa chama hicho kimekuwa kikiitenga Zanzibar katika masuala ya kiutawala na mgawanyo wa rasilimali.