Joy FM
Joy FM
10 October 2025, 21:35

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kubotesha miundombinu ya kujifunza na kufundishia ili kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewahimiza wazazi Mkoani Kigoma kuhamasisha watoto kuyapenda na kusoma masomo ya sayansi ili taifa liweze kuzalisha idadi kubwa ya watendaji watakalitumikia kupitia sekta zinazotegemea wataalam hao.
Balozi Sirro ametoa kauli hiyo alipokagua ujenzi wa maabara tatu kwa ajili ya masomo ya kemia, baiolojia na fizikia katika shule ya Sekondari ya Kakonko, ukiwa ni mradi uliotekelezwa na UNICEF kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa thamani ya shilingi milioni 180.
Amesema ni jukumu la wanufaika wa miundombinu hiyo muhimu ya kujifunzia na kufundishia kuitunza ili iweze kutumika kwa muda mrefu na kunufaisha kundi kubwa la watanzania.
Mkuu wa Shule hiyo Bi. Anatoria Paul amesema kukamilika kwa mradi kumeongeza hamasa kwa wanafunzi wengi kusoma masomo ya Sayansi sambamba na kufanya vizuri katika masomo hayo kutokana na utoshelevu wa vifaa vya kufundishia.

Anatoria ametoa shukurani kwa serikali ya awamu ya Sita kwa kushirikiana wadau wa Maendeleo kupitia Mpango wa pamoja wa Kigoma (KJP) kwa kukamilisha mradi huo ambao ambao pia utaongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.