Joy FM

Wawili mbaroni kwa mauaji ya dereva pikipiki Kigoma

21 April 2026, 10:42

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Filemon Makungu akionyesha baadhi ya vitu vilivyokuwa vimeibiwa, Picha na Esperance Ramadhan

Wananchi Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia na kuabaini vitendo vya uhalifu ili kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Na Esperance Ramadhan

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kumuua dereva bodaboda na kumnyang’anya pikipiki yake kabla ya kujaribu kutoroka kuelekea nchini Burundi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi  la Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Filemon Makungu amesema hayo wakati  akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya operesheni mbalimbali zilizofanyika moani Kigoma.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi  la Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Filemon Makungu

Aidha Kamada Makungu ameongeza kuwa kutokana na ushirikiano wa wananchi wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 283 ambao waliingia na kuishi nchini kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Filemon Makungu akionyesha pikipiki zilizokuwa zimeibiwa, Picha na Esperance Ramadhan

Hata hivyo baadhi ya wananchi Mjini Kigoma  wamesema kuwa ni muhimu Jeshi la Polisi kutengeneza mahusiano mazuri na wananchi ili waweze kutoa taarifa zinazohusu uhalifu unaofanywa kwenye jamii.  

Sauti ya Wananchi Kigoma

Oparesheni na misako ya kuzuia na kubaini uhalifu Mkoani Kigoma ilianza Machi 20, 2026 hadi Aprili 19,2026 katika Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kubaini wahalifu na wahamiaji haramu ambao wanaishi Mkoani Kigoma kinyume cha sheria.