Joy FM

Rais Dkt. Samia kuzindua meli nne za mizigo Kigoma

19 July 2026, 15:43

Katikati ni Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa na Mkuu wa Mkoa kigoma Simon Sirro, Picha na Josephinne Kiravu

Uzinduzi wa meli za mizigo ndani ya ziwa Tanganyika ni hatua muhimu ya kuufungua mkoa wa Kigoma sasa kuwa lango la kibiashara kwa nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika

Na Josephine Kiravu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua meli nne mpya za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 2000 kwa safari moja

Akitoa taarifa hiyo Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa amesema meli hizo ambazo zinatarijiwa kufanya safari zake ndani ya ziwa Tanganyika kutokea Kigoma kuwenda katika nchi za ukanda wa ziwa Tanganyika ikiwemo Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo ( DRC) Burundi ambazo zitakuwa na uwezo wa kubeba tani 832 kwa mwaka.

Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa Picha na Josephine Kiravu

​“Hatua hii itaufanya mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha usafirishaji na biashara kwa nchi za ukanda wa Ziwa Tanganyika,” alisema Waziri Mbarawa

Waziri amebainisha kuwa uzinduzi huo utachochea ongezeko la fursa za kiuchumi ikiwemo kuzalisha ajira mpya za moja kwa moja 600 wakiwemo madereva na wahudumu wa kwenye meli.

Katikati ni Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa na Mkuu wa Mkoa kigoma Simon Sirro, Picha na Josephinne Kiravu

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kigoma IGP mstaafu Balozi Simon Sirro amesema  kuwa, ujio wa meli hizo utatatua changamoto ya usafirishaji wa mizigo kuelekea nchini Congo DRC ambapo awali kulikuwa na ucheleweshaji wa shehena za mizigo kwa takribani miezi miwili.

Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro, Picha na Josephine Kiravu

Sambamba na uzinduzi wa meli hizo, Rais Samia ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha sita kutoka Tabora, kuelekea mkoani Kigoma inayogharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili.