Joy FM

Huduma ya M-mama yapunguza vifo vya mama na mtoto

10 September 2026, 18:16

Mwandishi wetu Emmanuel Kamangu akizungumza na mratibu wa M- mama Kasulu, Picha na Emmanuel Kamangu

Afya ya mama na mtoto ni jambo muhimu katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla miongoni mwa changamoto zinazoweza kuhatarisha maisha ya wajawazito na watoto ni kuchelewa kupata huduma za afya, hasa pale ambapo mgonjwa anahitaji usafiri wa haraka kwenda kituo cha afya.

Na Emmanuel Kamangu

Huduma ya  usafiri wa dharula kwa mama mjamzito na mama aliye jifungua yaani M-mama  katika halmashauri ya mji wa kasulu  imefanikiwa kupunguza vifo  vya mama na mtoto karibu kwa asilimia 90.

Akizungumz na redio joy  Bw, Augustin Karol ambaye ni Mratibu wa M-Mama katika halmashauri ya mji wa kasulu amebainisha kuwa  kwa miaka ya hivi karibuni jumla ya vifo 30 vya mama vitokavyo na uzazi  vimekuwa vikiibuliwa tofauti na hivi sasa ambapo  kuanzia January  mpaka septemba ya  mwaka huu 2026 ni vifo viwili pekee ambavyo vimeibuliwa.

Aidha Bw, Karoli amemtaka mama mjamzito kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya unaowataka kujali mda sahihi wa kiliniki ili kuendelea kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinakuwa historia.

Katika hatua nyingine  Bw, Karoli ameeleza kuwa uhaba wa magari na miundombinu ya babara mibovu kwa maeneo mengi ya vijijini imekuwa ni moja ya sababu inayopeleka mjamzito kuchelewa kufikishwa katika vituo vya afya hali inayohatarisha usalama wa mama na mtoto.

Hata hivyo Bw, Karoli amewataka wananchi  wanapoona hali ya hatari kwa mama mjamzito au mtoto mchanga kutumia namba  115 ambayo itasaidia watoa huduma kufika eneo husika kwa ajili ya msaada wa dharula.