Joy FM

UVINZA yaadhimisha mwezi wa maendeleo ya jamii

30 September 2026, 17:38

Baadhi ya watumishi Wilaya Uvinza wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya mwezi wa maendeleo ya jamii, Picha na Mwandishi wetu

Idara ya maendeleo ya jamii Wilayani Kasulu imetembelea miradi mbalimbali na kuwataka wananchi kutumia mikopo ya Halmashauri kujikwamua kiuchumi

Na Mwandishi wetu

Wataalamu wa kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Uvinza, leo septemba 30,2026 wamefanya ziara ya kuazimisha kilele cha mwezi wa Maendeleo ya Jamii kwa kutembelea mnada wa mwamila pamoja na mradi wa Bwawa la Samaki.

Katika ziara hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Uvinza Godfrid Nkuba ametoa wito kwa wananchi wote waliokidhi vigezo kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na Halmashauri, kwa upande mwingine amewataka kufichua ukatili wa kijinsia unaotendeka kwenye jamani zao na kuchukua tahadhari kuhusu magonjwa mbalimbali yanayoambukizwa kujamiana.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na wataalamu wa maendeleo ya jamii, Picha na Mwandishi wetu

Kwa upande mwingine wataalamu hao wametembelea mradi wa Kikundi cha Vijana Leo Mazungwe na kuwapongeza kwa juhudi zao ya uzalishaji wa Samaki, na kuweza kusambaza sehemu mbalimbali ikiwemo nje ya Wilaya.Aidha, Katibu mkuu wa Kikundi Ndg. Seif Haruna Kabiligi hicho amesema mradi huo ulianza mwaka 2022 ukiwa na mabwawa mwili na hadi kufika mwaka 2026 mradi huo umefikisha mabwawa 7.

Vilevile mradi huzalisha vifaranga vya samaki na kusambaza kwa wafungaji wa Samaki kwenye vituo 6 ambavyo ni Mganza ,Basanza, Mkuti, Lusesa, Mahembe pamoja na Kanyavu.

Nae Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Ezekiel Mafuru amewapatia wanakikundi mafunzo kuhusu namna Bora ya ufungaji wa Samaki na endapo ikijitokeza changamoto.