Joy FM
Joy FM
2 November 2026, 16:36

Serikali ya Mkoa wa Kigoma imekabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa kaya zilizoathirika na mvua
Na Josephine Kiravu
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari wakati mvua za elnino zikiendelea kunyesha ili kuepuka maafa yanayosababishwa na mvua hizo.
Ametoa wito huo wakati akitoa mahitaji ya kibinadamu kwa kaya zilizoathirika na mvua ya upepo iliyonyesha octobar 29, 2026 ambapo amesema ili kuondoka na madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha ni muhimu wananchi kuzingatia maelekezo waliyopewa.
Aidha Balozi Sirro ameendelea kwa kusema kuwa suaala la usafi wa mazingira na ukarabati wa nyumba ni njia bora zaidi ya kuepuka maafa hayo.
Kwaupande wao baadhi ya waathirika wa mvua hiyo wameishukuru serikali kwa kutoa msaada wa chakula na kuomba serikali kuwatafutia makazi mbadala ya kuishi baada ya kukubwa na kazia hiyo.