Joy FM

WPC yatoa cherehani kwa vijana ili kujiajiri Kigoma

20 November 2026, 12:51

Baadhi ya vijana wa kike waliopatiwa cherehani na Shirika la WPC, Picha na Shangwe Seluke

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kusaidia vijana kuweza kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri

Na Shangwe Seluke

Vijana kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na wadau wa maendeleo pamoja na kutumia vizuri ruzuku wanazopatiwa ili kufikia malengo waliyojiwekea na kujikwamua kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, katika hafla fupi ya ugawaji wa cherehani kwa vijana ambapo amewataka kuhakikisha wanatunza na kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili viweze kuwasaidia kujiajiri na kukuza shughuli zao za kiuchumi.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota

Baadhi ya vijana walionufaika na vyereheni hivyo wameakiwemo Amina Ahimad, wametoa shukrani kwa Shirika la WPC kwa kuwapatia vifaa hivyo, huku wakiwahimiza vijana wengine kutumia vizuri ruzuku na misaada wanayoipata katika kutekeleza shughuli walizokusudia.

Sauti za vijana

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Women Promotion Centre (WPC), Matha Jerome, ameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana na kuwafanya washindwe kujiajiri.

Sauti ya Mkurugenzi wa Shirika la Women Promotion Centre (WPC), Matha Jerome,

Aidha, ametoa mapendekezo ya namna ya kuboresha utoaji wa ruzuku ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika, huku akiwataka viongozi kushirikiana kwa karibu na vijana katika kutatua changamoto zao.