Joy FM

Watumishi wa umma watakiwa kuwaletea wananchi wananchi Kasulu

9 October 2026, 14:53

Alikuwa Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akiwa kwenye picha na wadau, Picha na Emmanuel Kamangu

Usimamizi madhubiti wa miradi unasaidia kuchochea maendeleo kwa wananchi

Na Emmanuel Kamangu

Watumishi wa umma Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha wanawaletea wananchi maendeleo.

Amebainisha hayo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanal Isack Mwakisu wakati akizungumza wanachama wa Timu Yanga ambao ni watumishi wa uma na wasio watumishi uma katika hafla maalumu ambayo wameiandaa kwa ajili ya kumuaga ambapo ametumia mwanya huo kuwasihi wakuu wa idara kuhakikisha wanashirikiana na viongozi wengine kukusanya mapato kwa masrahi ya wananchi.

Picha na Emmanuel Kamangu

Naye Kaimu mkurugenzi halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw, Emmanuel Ladslaus amempongeza Kanal Mwakisu kwanamuna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia maendeleo wilayani humo ikiwa ni pamoja na wananchi kufanya shuguli za uzalishji kwa amani na utulivu.

Aidha Mwenyekiti wa Timu ya Yanga halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw. Joseph Maiga kwa niaba ya wenzake amesema wamewiwa kumuaga Kanal Mwakisu kutokana na namuna ambavyo amekuwa akishiriki kikamilifu mambo ya kijamii pasipo ubaguzi jambo ambalo imekuwa rahisi wilaya ya kasulu kupiga hatua kimaendeleo.

Kanal Isack Mwakisu aliteuliwa na hayati Rais Dkt John pombe Magufuri kuja kuwa mkuu wa wilaya ya Kasulu mwaka 2021 na sasa Rais Dkt samia suruhu Hassan amemteua kuwa mkuu wa wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.