Joy FM

CP Mkama ataka usalama wa raia na mali zao kuimarishwa Kigoma

7 May 2026, 12:34

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama akisalimiana na askari mbalimbali mara baada ya kuwasili Kigoma na kupokelewa na RPC Kigoma SACP Filemon Makungu, Picha na Polisi Tanzania

Kikao hicho kinalenga kujadili namna bora ya kuendelea kushirikisha jamii katika masuala ya usalama na kuimarisha dhana ya polisi jamii katika maeneo yao

Na Mwandishi wetu

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama leo Mei 7,2026 amewasili Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ambapo amepokea taarifa ya hali ya usalama na kuwataka askari kuendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Akiwa Mkoani Kigoma atafanya kikao kazi na viongozi wa Serikali za mitaa/Vijiji, Kata na viongozi wa dini na Polisi kata kwa lengo la kuhamasisha jamii kuendelea kutii sheria bila shuruti na kushiriki kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu.

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama akisalimiana na askari mbalimbali mara baada ya kuwasili Kigoma na kupokelewa na RPC Kigoma SACP Filemon Makungu, Picha na Polisi Tanzania

Sambamba na hilo, CP Mkama amehimiza wananchi kuendelea kutii sheria bila kushurutishwa na kushiriki kikamilifu katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu.

Amesema usalama wa nchi ni jukumu la kila mwananchi, hivyo ni muhimu jamii kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kudhibiti vitendo vya uhalifu kabla havijatokea au kuleta madhara kwa jamii.

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama akiwa amewasili Kigoma na hapa ni katika Ofisi ya RPC Kigoma aliyesimama ni RPC Kigoma SACP Filemon Makungu, Picha na Polisi Tanzania