Joy FM

Vikundi vya ulinzi shirikishi vyapunguza uhalifu Kasulu

20 May 2026, 13:03

Mtaa wa Umoja katika kata ya Murubona, Picha na Hagai Ruaygila

Ulinzi shirikishi ni mfumo wa usalama unaohusisha ushirikiano kati ya wananchi, vyombo vya dola na viongozi mbalimbali katika kuhakikisha jamii inakuwa salama muda wote na mfumo huu unalenga kuwafanya wananchi kuwa sehemu ya ulinzi wa maeneo yao badala ya kuacha jukumu hilo kwa polisi pekee

Na Hagai Ruyagila

Hali ya ulinzi na usalama katika kata ya Murubona Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma imeendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuundwa kwa vikundi vya ulinzi shirikishi vinavyofanya doria usiku na machana katika mitaa mbalimbali ndani ya kata hiyo.

Akizungumza na Vyombo vya habari, Diwani wa Kata ya Murubona, Mh Jumanne Mustafa, amesema hapo awali hali ya ulinzi na usalama ilikuwa tete kutokana na matukio ya ukabaji na uvunjaji wa nyumba nya kati za usiku.

Diwani wa kata ya Murubona, Picha na Hagai Ruyagila

Amesema baada ya kuanzishwa kwa vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi, matukio hayo yamepungua kwa kiwango kikubwa.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Murubona, Mh Jumanne Mustafa Radio JOY Profile

Mwenyekiti wa mtaa wa Umoja, Richard Martine amesema kwasasa wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kwa amani, hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi wa serikali pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa mapema wanapobaini viashiria vya uhalifu.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Umoja, Richard Martine
Mwenyekiti wa mtaa wa Umoja, Picha na Hagai Ruyagila

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Murubona wamesema mfumo wa ulinzi shirikishi umeleta mafanikio makubwa katika kupunguza vitendo vya uhalifu vilikuwa vinajitokeza hapo awali, hali ambayo imeongeza utulivu na kuimarisha usalama katika maeneo yao.

Sauti za wananchi Kasulu