Joy FM

Injini mbili zawasili kwa ajili ya ukarabati wa Mv. Liemba Kigoma

14 Aprili 2026, 13:00

Muonekano wa Meli ya Mv. Liemba ambayo ipo kwenye ukarabati, Picha na Mtandao

Ukarabati wa Mv. Liemba unaonekana kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi, hususan kwa wakazi wa maeneo ya kandokando ya Ziwa Tanganyika ambao hutegemea kwa kiasi kikubwa usafiri wa majini kwa shughuli zao za kila siku

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 32 kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa Meli ya kihistoria ya Mv. Liemba.

Shukrani hizo za Mkuu wa Mkoa Balozi Simon Sirro kwa Rais, zimetolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua, wakati alipomwakilisha kwenye mapokezi ya Injini mbili zilizofika kwa ajili ya kukamilisha ukarabati mkubwa wa Meli ya Mv.Liemba katika Bandari ya Kigoma.

Amesema hatua hiyo inaashiria historia mpya kwa wana Kigoma kwenye sekta ya usafiri na usafirishaji katika Ziwa Tanganyika, baada ya miaka kadhaa ya kusimama kwa Meli ya Mv.Liemba bila kutoa huduma.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua

Meneja Mradi wa Ukarabati wa Meli ya Mv. Lemba Mhandisi Elias John Kivala, ukarabati wa meli hiyo umefikia asilimia 64%, na kwamba mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Sauti ya Meneja Mradi wa Ukarabati wa Meli ya Mv. Lemba Mhandisi Elias John Kivala

Kwa upande wao Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Sadick Kibwana Kadulo, pamoja na Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Musa Maulid, wamesema meli hiyo ni mkombozi kwa wananchi wa Kigoma kwenye masuala ya usafiri na uchumi.

Sauti ya Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Sadick Kibwana Kadulo, pamoja na Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Musa Maulid