Joy FM

Wakristo waaswa kumtegemea Mungu katika maisha yao Misenyi

1 January 2026, 14:19

Waumini wa Kanisla la KKKT baada ya ibada ya Mwaka mpya 2026 Usharika wa Kikukwe Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Picha na Hagai Ruyagila

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kikukwe Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mchungaji Edward Mutashobya amesema kumtegemea mungu kunasaidia kuendelea kuwa maisha yaliyo mema.

Na Hagai Ruyagila

Waumini wa dini ya Kikristo Wilayani Misenyi mkoani Kagera wametakiwa kumtegemea Mungu katika maisha yao ya kila siku, licha ya mipango wanayojiwekea katika mwaka mpya wa 2026.

Wito huo umetolewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kikukwe Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mch. Edward Mutashobya wakati akihubiri neno la Mungu katika ibada ya sikukuu ya mwaka mpya kanisani hapo.

Mchungaji Mutashobya amesema kuwa ili kuhakikisha mafanikio yao yanakuwa salama na endelevu, waumini wanapaswa kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika mipango yao yote.

Ameongeza kwa kusema kuwa kumtegemea Mungu kutawasaidia kufanya maamuzi sahihi na kuepuka changamoto zisizo za lazima.

Sauti ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kikukwe Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mch. Edward Mutashobya
Mchungaji kiongozi wa usharika wa Kikukwe Wilaya ya Misenyi, Picha na Hagai Ruyagila

Aidha, amewahimiza waumini kuzingatia afya zao kwa kufanya uchunguzi wa kiafya mara kwa mara, angalau kila baada ya miezi mitatu, ili kubaini mapema changamoto za kiafya na kuchukua hatua stahiki.

Sauti ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kikukwe Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mch. Edward Mutashobya

Kwa upande wao, baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamesema mafundisho hayo yamewapa mwanga na hamasa ya kuanza mwaka mpya kwa kumuamini Mungu zaidi, huku wakizingatia pia afya na mipango yao ya maendeleo binafsi.