Joy FM
Joy FM
23 July 2026, 15:41

Halmashauri zina jukumu la kusimamia maendeleo na kutoa huduma muhimu kwa wananchi katika maeneo yao na ili ziweze kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi zinahitaji kuwa na rasilimali za kutosha za kifedha na hivyo uanzishwaji wa vyanzo vipya vya mapato ni kuongeza uwezo wa kifedha na kuboresha utoaji wa huduma.
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyoiwezesha halmashauri hiyo kukua kiuchumi
Balozi Sirro amesema hayo kupitia kikao cha baraza maalumu la madiwani cha kuwasilisha utekelezaji wa hoja za mdhibiti na mkuaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kuhusu ukaguzi wa tatarifa za fedha kwa mwaka 2025/26
Amesema zipo fursa mbalimbali zikiwemo za kilimo cha mazao ya biasha kama vile zao la mhongo ambalo likisimamiwa vyema huweza kuinua uchumi wa wananchi na halmashauri.
Naye mkuu wa wilaya ya Kibondo Kanali mstaafu Aggrey Magwaza amesema amesema wataendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha uchumi wa halmashauri unaendelea kukua