Joy FM
Joy FM
11 August 2026, 13:18

Watoto wa kikie wanatakiwa kuwekewa mazingira weshezeji kwa ajili kusoma na kutimiza ndoto zao.
Na Hagai Ruyagila
Taasisi ya Shukrani Foundation imetoa vifaa vya shule vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa wasichana 50 wa shule za msingi na Sekondari katika Halmashauri ya mji Kasulu Mkoani kigoma kwa lengo la kuwahamasisha kuhudhuria masomo shuleni.

“Nguvu ya Binti ipo Kwenye Elimu” ni kauli mbiu ambayo hutumiwa na taasisi ya shukrani Foundation inayolenga kuwahudumia watoto wa kike katika masuala mbalimbali na hapa mkurugenzi wa taasisi hiyo Bi.Josephina Alphonce anaeleza kile ambacho wamekitoa kwa wanafunzi hao.
Mkuu wa shule ya Bogwe Sekondari Mwl David Kindanda amesisitiza wazazi kuacha ulevi wa kupindukia badala yake wanatakiwa kutimiza mahitaji muhimu kwa watoto wao.
Mgeni rasmi katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo vya Shule ambaye ni mkuu wa shule ya Sekondari kidyama Amisa Juma Rajabu amesema wazazi wanatakiwa kuimarisha ulinzi kwa watoto wao na kujenga ukaribu nao.

Baadhi ya wazazi wa watoto waliopatiwa vifaa hivyo wameeleza kuwa itawasaidia watoto katika masomo yao.