Joy FM

“Madiwani wekeni kando tofauti zenu za kisiasa” DC Kasulu

28 April 2026, 11:50

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Kuweka tofauti pembeni kunasaidia kuleta maendeleo ya haraka, endelevu na yenye kuwanufaisha wananchi wote

Na Hagai Ruyagila

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isaac Mwakisu, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kuweka tofauti zao za kisiasa badala yake wametakiwa kushirikiana na Wananchi wa wao katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Kanali Mwakisu ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na Madiwani, Viongozi wa Umma pamoja na viongozi wa vyama vya siasa katika ukumbi wa mikutano wa Kagoma uliopo makao makuu ya halmashauri hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isaac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila

Amesema uchaguzi umeshamalizika, hivyo ni muhimu kwa viongozi hao kushirikiana kwa pamoja kudumisha umoja na mshikamano ili kusimamia rasilimali za umma na kutatua changamoto za wananchi kwa wakati hatua itakayosaidia kupeleka maendeleo kwa jamii.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isaac Mwakisu

Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mh. Charles Benjamini, amesema kumekuwepo na mivutano kwa viongozi wa kata hiyo, hali inayopeleka migogoro na kushindwa kutekeleza majukumu yao, hivyo amesema serikali itachukua hatua ya kutatua changamoto hiyo ili kuwasaidia wananchi kupata maendeleo.

Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mh. Charles Benjamini, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Mh. Charles Benjamini

Diwani wa viti maalum kata ya Makere, Mh Mwasi Mchunga, amesema ni kata baadhi ndiyo bado wanaendelea na changamoto ya makundi licha ya uchaguzi mkuu kutamatika hivyo ni wakati wa kuyaondoa makundi hayo ili viongozi waliochaguliwa waweze kuwatumikia wananchi waliowachagua.

Sauti ya Mh Mwasi Mchunga