Joy FM

Ukatili wa kiuchumi kikwazo wanawake kufikia ndoto zao Kigoma

28 May 2026, 11:38

Baadhi ya wanawake wajariamalia wakizungumzia madhira ya ukatili wa kiuchumi unaathiri maendeleo ya wananwake, Picha na Tryphone Odace

Ukatili wa kiuchumi ni aina ya ukandamizaji ambapo mtu mmoja humzuia mwingine kupata, kutumia au kumiliki rasilimali za fedha na mali au kutoshirikishwa katika maamzi ya kiuchumi kwa familia.

Mara nyingi wanawake na wasichana hukumbwa na ukatili huu katika familia, jamii na hata sehemu za kazi, ukatili wa kiuchumi unaweza kujitokeza kwa njia mbalimbali kama kunyimwa haki ya kufanya kazi, kupokonywa kipato, kuzuiwa kusoma au kurithi mali, pamoja na kulazimishwa kutegemea wanaume kwa mahitaji yote ya msingi.

Msikilizaji kipindi hiki kimeletwa kwako kwa ushirikiano wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa ushirikiano na Mtandao wa redio za kijamii Tanzania TADIO.

Sikiliza Makala inayohusu ukatili wa kiuchumi kwa wanawake na madhara yake