Joy FM
Joy FM
11 November 2024, 14:02

Wahitimu wa mafunzo ya biblia katika chuo cha biblia Dar es salaam tawila Kigoma wametakiwa kuisaidia jamii kuachana na vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikifanyika na kusababisha baadhi ya makundi mbalimbali kuathirika ikiwemo ukatilii na uvunjifu wa amani.
Na Timotheo Leonard – Kigoma
Chuo cha mafunzo ya Biblia Dar es salaam tawi la Kibirizi Mkoani Kigoma kimepanga kuendelea kupanua wigo wa kuwapa nafasi wanafunzi kujifunza Biblia kabla ya kuanza uinjilishaji.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa chuo hicho Askofu Dokta Fredrick Simon katika mahafari ya kuhitimu elimu ya biblia kwa wanafunzi 19 wa ngazi ya cheti na Diploma iliyofanyika katika kanisa la MMPT Pentekoste Kibirizi na kuwa wale ambao hawajajiunga na mafunzo ya Biblia hawana budi kusoma ili kulielewa vema neno la Mungu.
kwa upande wake, Mwalimu Ladislaus Kilasa ambaye amekuwa akiwafundisha wanafunzi hao amesema anamatarajio makubwa kwa wanafunzi kutokana na maarifa waliyoyapata.
Kwa upaande wake, Jamilu Athumani Halfani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafari hiyo ameahidi kutoa vifaa mbalimbali vya ujenzi wa darasa litakalosaidia chuo hicho kupokei wanafunzi wakutosha kujifunza Biblia.
Nao baadhi ya wahitimu wa chuo hicho wamesema taaluma waliyoipata wataitumia vizuri.
Aidha wanafnzi waliohitimu ni 19, ngazi ya cheti wakiwa 7 na Diploma 12 hii ikiwa ni mahafari ya tatu toka chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 2021.