Joy FM

UHDO yataka maeneo ya kihistoria Kigoma yahifadhiwe

23 June 2026, 09:52

Baadhi ya washiriki wa kongamano la urithi wa Mji mkongwe wa Ujiji, Picha na Lucas Hoha

Maeneo ya kihistoria na urithi wa kitamaduni ni sehemu muhimu ya utambulisho wa taifa na jamii na maeneo haya huhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu yaliyotokea zamani na hutusaidia kuelewa historia ya nchi yetu

Na Lucas Hoha

Mwenyekiti wa Taasisi ya Ujiji Heritage and Development Organization (UHDO) iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji, Shehe Hassan Kabeke, amezitaka mamlaka za serikali za mitaa na Serikali Kuu kuyatambua, kuyahifadhi na kuyalinda maeneo ya kihistoria ambayo yameanza kupotea kutokana na shughuli za ujenzi zinazoendelea.

Kabeke, ambaye pia ni Shehe wa Mkoa wa Mwanza, amesema hayo alipokuwa akitoa salamu kwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid, katika Tamasha la Utamaduni lililofanyika mjini Kigoma.

Kabeke ambaye pia ni Shekhe wa Mkoa wa Mwanza, Picha na Lucas Hoha

Ametaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pamoja na yale aliyowahi kufikia Baba wa Taifa, Julius Nyerere, wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanzania.

Sauti ya Shehe wa Mkoa wa Mwanza

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid, amesema historia na utamaduni wa Ujiji ni wa kipekee. Aidha, amewataka wazazi kusimamia maadili mema katika jamii na kukemea vitendo vinavyokiuka maadili ya jamii.

Sauti ya Meya wa Manispaa
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid, Picha na Lucas Hoha

Naye baadhi ya washiriki wa mkutano huo waliozaliwa Mkoa wa Kigoma wamesema wazaliwa wa mkoa huo wanapaswa kuwekeza nyumbani kwao ili kuongeza fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi.

Sauti ya Washiriki wa mkutano