Joy FM
Joy FM
22 April 2026, 17:43

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la ujenzi wa makazi katika maeneo yanayokumbwa na maji kutuama, hasa katika miji inayokua kwa kasi, licha ya ongezeko la mahitaji ya ardhi ya makazi, wataalamu wanaonya kuwa kujenga nyumba katika maeneo hayo kunaweza kuleta madhara makubwa kwa wakazi na mali zao.
Na Lucas Hoha
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka wananchi kuacha kujenga nyumba katika maeneo ambayo yana tabia ya kujaa maji ili kuepuka athari za mafuriko yanayotokana na mvua na kusababisha maafa.
Balozi Sirro ameyasema hayo wakati akigawa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mchele na sukari vyenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwa waathirika wa mafuriko katika kata ya kimpampa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashird Chuachua amesema tangu mvua kunyesha na kusababisha adha hiyo wamekuwa wakiwatembelea wananchi hao na kutoa elimu ya masuala ya kisaikolojia, huku mratibu wa maafa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Kigoma Ujiji Joseph Malugo akifafanua nyumba zilizoathirika na hatua zilizochukuliwa.

Wakizungumza na Radio Joy fm, Baadhi ya wahanga wa mvua hiyo ambao wamepokea msaada huo, wameshukuru serikali kwa kuwajali kutokana na adha waliyokumbana nayo.
Mvua hiyo iliyonyesha siku chache zilizopita iliambatana na upepo mkali ambapo ilisababisha adha kwa kaya zaidi ya kaya 100 na wengine wamelazika kuhama makazi yao kutokana na nyumba kubomoka