Joy FM

DC Kasulu ataka wazazi kuwainua watoto kiuchumi

23 June 2026, 10:30

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu, Picha na Mwandishi wetu

Wazazi na walezi wana jukumu kubwa la kuwalea na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye mbali na kuwapatia elimu na mahitaji muhimu, ni muhimu pia kuwawezesha kiuchumi ili waweze kujitegemea na kuchangia maendeleo ya familia na jamii

Na Mwandishi wetu

Wazazi na walezi wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuwawezesha watoto wao kiuchumi kwa kuwapatia mitaji na kuwaunga mkono katika kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji mali ili waweze kujitegemea.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu, wakati akizungumza na wananchi wilayani humo na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwawezesha watoto wao kiuchumi ili waweze kuwa sehemu ya maendeleo ya familia.

Kanali Mwakisu amesema wazazi wanapaswa kuwapa ushirikiano, ushauri na kuwawezesha kuanzisha shughuli za uzalishaji mali kulingana na vipaji, ujuzi na uwezo wao.

Sauti ya Mkuu wa Wilya Kasulu

Baadhi ya wananchi wilayani kasulu wamesema wito huo utasaidia kuhamasisha vijana wengi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kujenga utamaduni wa kujitegemea.