Joy FM

Wananchi walia umeme kutokuwa na nguvu Kagunga

16 April 2026, 2:45 pm

Muonekano wa mfumo wa umeme, Picha na Mtandao

Upatikanaji wa umeme wa kutosha ni moja ya nguzo muhimu katika maendeleo ya kisasa ya jamii yoyote na Umeme unapokuwa wa uhakika na wa kutosha, huchochea ukuaji wa uchumi, huboresha huduma za kijamii, na kuinua kiwango cha maisha ya watu.

Na Orida Sayon

Wananchi wa mtaa wa Makombe kijiji cha Kagunga Halmashauri ya wilaya ya Kigoma wameliomba Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa kigoma kusaidia kutatua changamoto ya umeme katika kitongoji hicho.

Wakizungumza na Radio Joy Fm, Wananchi hao wa kitongoji cha makombe kijiji cha kagunga wamesema kwa siku kadhaa huduma ya umeme iliyopo inasaidia kwa matumizi madogo madogo hali inayokwamisha shughuli za maendeleo hasa uchomeleaji unaohitaji nguvu ya umeme.

Sauti ya Wananchi wa mtaa wa Makombe kijiji cha Kagunga Halmashauri ya wilaya ya Kigoma

Naye Kaimu afisa mtendaji wa kata na kijiji cha Kagunga Augostino Joseph amewataka wananchi hao kuwa watulivu na kwamba wanaendelea kulifanyia kazi ili kuweza kutatua changamoto hiyo kwa kushirikiana na TANESCO.

Sauti ya Kaimu afisa mtendaji wa kata na kijiji cha Kagunga Augostino Joseph

Kufuatia changamoto hiyo, Radio Joy Fm imeutafuta uongozi wa TANESCO Mkoa wa Kigoma ili kufahamu nini changamoto na wana mkakati upi ambapo Afisa Uhusiano TANESCO mkoa wa kigoma Bernad Mafuru anaeleza.

Sauti ya Afisa Uhusiano TANESCO mkoa wa kigoma Bernad Mafuru