Joy FM
Joy FM
6 August 2026, 09:45

Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote kinachosababisha madhara ya kimwili, kingono, kisaikolojia au kiuchumi kwa mtu kutokana na jinsia yake na suluhu za kifamilia ni jitihada zinazofanywa na wanafamilia, wazee wa ukoo au viongozi wa jamii kutatua migogoro bila kutumia mfumo rasmi wa sheria.
Na Mwandishi wetu
Ili kuhakikisha manusura wanapata haki ni muhimu kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na umuhimu wa kuripoti matukio kwa mamlaka husika na serikali na wadau wanapaswa kuimarisha huduma za afya, msaada wa kisaikolojia, ushauri wa kisheria na ulinzi kwa manusura.