Joy FM
Joy FM
16 July 2026, 16:49

Utekelezaji wa mradi wa uhifadhi wa mazingira katika vijiji vinne vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Makere Kusini na pori la Akiba la Moyowosi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, unaotekelezwa na Shirika la TAWEA, umetajwa kuleta mabadiliko chanya katika shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika vijiji hivyo.
Mradi huo umeendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda rasilimali za asili, hatua inayochangia kuimarisha uhifadhi wa mazingira pamoja na kupunguza vitendo vya uharibifu wa misitu na wanyamapori katika maeneo ya vijiji vya Kagerankanda,Mvinza,Chekenya na Kabulanzwili ambako mradi huo unatekelezwa.
Akizungumza katika warsha na wadau wa uhifadhi wa mazingira na uhifadhi wa misitu na wanyamapori Halmashauri ya wilaya ya Kasulu mratibu wa mradi huo kutoka shirika la TAWEA Bw.Batro Ngilangwa amesema mpaka sasa katika mradi huo wa miaka mwili umeleta manufaa makubwa kwa wananchi ikiwa mwaka mmoja tangu ulipoanza kutekelezwa.

Misitu ni rasilimali muhimu inayochangia maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii na wananchi wana wajibu mkubwa wa kulinda misitu kwa sababu ndiyo chanzo cha faida nyingi za kiuchumi, kijamii na kimazingira
Na Mwandishi wetu
Kwa upande wake Mhifadhi wa Pori la Akiba la Moyowosi kutoka Mamlaka ya usimamizi wanyamapori Tanzania TAWA bw.John kanyika amesema kupitia mradi huo wa TAWEA kwa kushirikiana na wananchi katika uhifadhi wa misitu na wanyamapori wameendelea kutatua changamoto na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaonufaika na mradi Huo.
Mdau wa uhifadhi wa mazingira kutoka shirika la TAWEA Alfan Ntayomba amesisitiza ushirikiano wa mamlaka za usimamizi wa misitu na wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Kasulu katika kufikia malengo ya mradi pamoja na kuimarisha uhifadhi na utunzaji wa misitu.
Mradi wa uhifadhi na utunzaji wa mazingira unatekelezwa katika vijiji vinne vinavyozunguka hifadhi ya msitu wa makere kusini,na Pori la akiba la Moyowosi na ugharimu Euro Laki 1 ukitarajiwa kutamatika mwaka 2027.