Joy FM

Madiwani watakiwa kutoa elimu ya usalama Kasulu

5 May 2025, 12:28

Madiwani katika halmashauri ya mji wa Kasulu wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani, Picha na Hagai Ruyagila

Viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji wametakiwa kusaidia kuwaelesha wananchi juu ya usalama katika maeneo yao

Na Hagai Ruyagila-Kasulu

Madiwani wa halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kutoa elimu ya usalama katika maeneo yao hii ni kutokana na hali ya usalama kwa baadhi ya maeneo kutajwa kuteteleka kutokana na viashiria vya wakimbizi au wahamiaji haramu kuingia katika wilaya hiyo kinyume na utaratibu.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu wakati akitoa salamu za serikali katika mkutano wa baraza la madiwani halmashauri ya Mji Kasulu robo ya tatu kipindi cha Januari mpaka Machi mwaka wa fedha 2024/2025.

Kanal Mwakisu amesema moja ya kata inayoguswa na uingiaji kihorera wa Wakimbizi kutoka nchi nyingine ni kata ya Muhunga ambapo hapa akatoa wito kwa madiwani kutoa elimu ya usalama katika maeneo yao.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu
Madiwani katika halmashauri ya mji wa Kasulu wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani, Picha na Hagai Ruyagila

Afisa mtendaji wa kata ya Muhunga Dorcas Swai anaeleza namna hali ya usalama ilivyo na mpango wa kukabiliana na hali hiyo.

Sauti ya Afisa mtendaji wa kata ya Muhunga Dorcas Swai

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji Kasulu wamezungumzia namna ambavyo jamii kwa kushirikiana na serikali wanaweza kuhakikisha usalama unaendelea kuimarika katika halamashauri hiyo.

Sauti ya Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji Kasulu
Maafisa Watendaji wa kata kutoka halmashauri ya Mji wa Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila