Joy FM
Joy FM
18 May 2026, 14:13

Katika jamii yoyote yenye utulivu, maendeleo na usalama ni jambo muhimu sana na hivyo wananchi kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu na wahalifu na ushirikiano huu una nafasi kubwa katika kudumisha amani, usalama na maendeleo ya taifa
Na Orida Sayon
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limewakata watuhumiwa wanne wakiwa na pikipiki tano zinazodhaniwa kuwa mali ya wizi.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma SACP Filemon Makungu wakati akizungumza wa wandishi wa habari foisni hii leo, kuhusu mafanikio ya misako na operesheni mbalimbali zinazoendelea katika wilaya zote za mkoa wa Kigoma.
Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni zilizofanyika mwezi April 20, 2026 waliweza kukamata wanne wakiwa na pikipiki hizo ambapo pia huko Wilayani uvinza kijiji cha Mwakizega Jeshi hilo limewakamata mtuhumiwa akiwa na noti bandia 85 za Tsh. 10,000/=

Aidha Kamanda Mkaungu amebainisha kuwa April 25, 2026 Wilayani Kasulu Askari Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya usimamizi wa wanyapori Tanzania walikamata mtuhumiwa mmoja akiwa na nyara za serikali huku mnamo Mei 13 katika kijiji cha Magarama wilaya ya kibondo walifanikiwa kukamata watuhumiwa watatu wakisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linaendelea kutoa rai kwa wananchi mkoani kigoma kushirikiana na jeshi hilo katika kuzuia na kubaini uharifu kwa lengo la kuimarisha usalama wa raia na mali zao.