Joy FM
Joy FM
10 October 2024, 16:58

Shirika la Plantvillage limesema linatarajia kupanda miche ya migomba kwenye eneo la ekari 32 itakayokuwa inatumika kwa wakulima ili kupunguza migamba inashambuliwa na magonjwa.
Na Michael Mpunije – Buhigwe
Katika kukabiliana na ugonjwa wa Funga shada ya Migomba ambao umeshambulia kwa kiasi kikubwa zao la migomba wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma shirika la Plantvillage Tanzania limepokea miche safi ya migomba elfu 29 ambayo inatarajia kusambazwa kwa wakulima wa zao hilo wilayani humo.

Shirika hilo la plantvillage ambalo linafadhiliwa na watu wa marekani la USAID limesema miche hiyo ya migomba inatarajiwa kupandwa kwenye mashamba yenye ukubwa wa ekari 32 kwa lengo la kurejesha hali ya uzalishaji wa zao la migomba wilayani Buhigwe kama anavyoeleza kiongozi wa mradi kutoka shirika la plantvillage bw.Joakimu Gobanya.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Bw.Alphonce haule amesema uzalishaji wa zao hilo umeshuka kwa kiasi kikubwa wilayani humo baada kushambuliwa na ugonjwa wa funga shada ya migomba.

Martin kasiano na Norbeth mahinini ni baadhi ya wakulima wazao la migomba kutoka wilayani Buhigwe ambao wanaeleza namna watakavyonufaika na miche hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya maafisa kilimo wa shirika la plantvillage kutoka kata ya mkatanga Bw.Experius Mrefu na Anjelina Samweli kutoka kata ya Buhigwe wamesema watahakikisha wanawasimamia wakulima na kuendelea kutoa elimu ili waweze kuzalisha kwa wingi ili kupata chakula na kukuza uchumi wao.
