Joy FM

Wafanyabiashara waaswa kujiunga TNCC kukuza mitaji Kigoma

9 October 2026, 11:25

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua akizungumza katika kikao cha wafanyabiashara, Picha na Sadick Kibwana

Biashara ni mojawapo ya shughuli muhimu zinazochangia ukuaji wa uchumi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla hata hivyo, changamoto kubwa inayowakabili wafanyabiashara wengi ni kushindwa kukuza mitaji yao kutokana na matumizi yasiyo na mpangilio, usimamizi duni wa fedha na kukosa mikakati madhubuti ya kuendeleza biashara zao

Na Sadick Kibwana

Wafanyabiashara Mkoani Kigoma wameaswa kujiunga na chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) ili kukuza mitaji na kufikia fursa nyingi zaidi za kibiashara.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, katika Kikao cha Kimkakati cha Wadau wa Biashara kilichoratibiwa na Ofisi ya TNCC Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua akiwa kwenye picha na wafanyabiashara na viongozi

Dkt. Chuachua amesema serikali inaendelea kuboresha miundombinu ili kufungua fursa zaidi za maendeleo kwa wananchi.

Aidha, Mwenyekiti wa Chemba ya Taifa ya Biashara mkoani hapa Obadia Kabuga amesema jukwaa hilo limekutanisha mashirika na wadau mbalimbali ili kuweka mikakati ya kuwainua wananchi kiuchumi.

Baadhi ya wafanyabiashara, Picha na Sadick Kibwana

Kwa upande wao, washiriki wa kikao hicho wameeleza manufaa makubwa ya elimu waliyoipata na jinsi itakavyosaidia kuboresha biashara zao.

Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC), ambayo zamani ilijulikana kama TCCIA tangu kuanzishwa kwake mwaka 1988, inaendelea kuwa kiungo muhimu kati ya sekta binafsi na serikali katika kukuza uchumi wa nchi.