Joy FM

DC Kasulu ahimiza utunzaji wa mazingira

17 November 2026, 10:33

Mkuu wa Wilaya Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Wadau mbalimbali wameendelea kuhimiza utanzaji wa mazingira kwa kupanda miti.

Na Hagai Ruyagila

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Luten kanali Joseph Murimi amewataka wananchi wilayani humo kuzingatia uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwalimu akikabidhiwa bendera ya Halmashauri, Picha na Hagai Ruyagila

Ametoa wito huo wakati akizungumza katika hafla ya Kumuaga mwl.Wenseslaus Lugaya ambaye ameanza safari ya kutembelea mikao 31 ya Tanzania bara na visiwani kwa kutumia usafiri wa Baiskeli kutokea wilayani Kasulu kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Luten Kanali Murimi amesema kwasasa dunia inashuhudia athari za mabadiliko ya tabia nchi kutokana na changamoto ya uhifadhi wa mazingira ambapo amesisitiza jamii kupanda miti katika maeneo yao.

Baadhi ya watumishi wa wakiongozwa na Dc Kasulu wakati wa kumuaga Mwalimu huyo, Picha na Hagai Ruyagila

Kwa upande wake mwl Wenseslaus Lugaya amesema katika safari hiyo atatembelea mikoa 26 ya Tanzania Bara na mikao 5 ya Visiwani Zanzibar sawa na umbali wa kilomita 8721 kwa kutumia usafiri wa Baiskeli ambapo safari hiyo imeanza rasmi leo novemba 16,2026 na kutamatika Februari 16,2027 kwa lengo la kuhamasisha upandaji wa miti milioni moja laki 5 na elfu ishirini.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu, Nurfus Aziz Ndee amesema mwalimu Wenseslaus Lugaya ana uzoefu wa safari ndefu kwa kutumia baiskeli ya magurudumu mawili.