Joy FM

Theluthi ya wazee nchini wanaishi chini ya msitari wa umasikini

29 October 2026, 15:24

Afisa lishe Mkoa wa Kigoma James Ngaraba, Picha na Filbert Gabriel

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo hawana budi kuendelea kuweka mazingira na wezeshi ili kuwasaidia wazee kwa ajili ya ustawi wao kwa kuboresha huduma ikiwemo malazi

Na Filbert Gabriel

Wazee ni kundi la watu waliosahaulika katika mambo mengi ambapo theluthi moja ya wazee wote Tanzania wanaishi chini ya msitari wa umasikini wa mahitaji ya msingi na 14% hawana chakula cha kutosha na hivyo kukabiliwa na tatizo la utapiamlo huku wanawake wazee wakiwa wahanga zaidi.

Kutengwa na imani za kishirikina, umasikini, kutelekezwa na familia na ukosefu wa bima za afya ni baadhi ya sababu zinazopelekea wazee hawa wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kukosa lishe bora na hivyo kuhatarisha ustawi wao.

Kundi hili la Wazee linahitaji kupata lishe bora ya vyakula kutoka katika makundi 6 ambayo ni wanga, Protini, vitamini, mafuta na sukari kidogo sana, madini na maji.

Afisa lishe Mkoa wa Kigoma James Ngaraba anatueleza namna Wazee wanavyotakiwa kupata lishe bora kwa ustawi wa afya zao.

Mtindo wa maisha ni moja ya hali tishio sana kwa Kundi hili la wazee, na hivyo kundi hili wanapaswa kuepuka vyakula visivyofaa kama vile vyakula vyenye sukari nyingi kama ambavyo afisa lishe anavyobainisha.

Pamoja na hayo afisa lishe Mkoa wa Kigoma James Ngalaba amekiri kuwa kundi hili limesahaulika na akaeleza kile walichoanza kufanya.

Jumanne Hussein Fumawicha, ana umri wa miaka 82 anapitia changamoto ya sukari na alipogundua tatizo hilo alibadili mfumo wa maisha na anafanya kazi zake akiwa na nguvu za kutosha, Na hapa anatusimuliana namna anavyopata na kupangilia mlo wake wa siku.

Wazee ni tunu,wazee ni hazina,wazee ni baba, mama, babu na bibi zetu, tuwatunze