Joy FM
Joy FM
19 November 2026, 14:53

Matumizi ya vipimo imeendelea kuwaathiri kiuchumi wakieleza kuwa matumizi ya lumbesa yamekuwa yakiwarudisha nyuma.
Na Josephine Kiravu
Wakulima katika Kata Matendo Halmashauri ya wilaya ya Kigoma wameiomba Serikali kuwashughulikia wanunuzi wa mazao yao ambao wamekuwa wakikaidi kutumia vipimo vinavyotakiwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema wanalazimika kuuza kwa hasara mazao yao ikiwemo mafuta ya mawese kutokana na kukosekana kwa kipimo kinachoruhusiwa kutumika eneo la soko.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Matendo Wiliam Mozes amekiri uwepo wa changamoto hiyo kwa wakulima na kuzitaka mamlaka husika kuchukua hatua kwa wanunuzi wasio waaminifu.
Meneja wakala wa vipimo mkoani Kigoma Laurent Kabikiye amekiri uwepo wa baadhi ya wafanyabiashara ambao hawatumii vipimo vinavyotakiwa na ameahidi kupeleka vipimo kwa ajili ya wauzaji wa mafuta ya mawese huku akisistiza wauzaji na wanunuzi kuacha kutumia kipimo maarufu kwa jina la bidoo kwani kipimo hicho hakitambuliki na kinampunja mkulima.

Akizungumzia kuhusu mazao ya nafaka na dagaa amewataka wauzaji kutumia mizani ya kisasa na kuachana na ile ya zamani ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wateja wao.
Itakumbukwa kuwa akiwa mkoani Kigoma mwaka 2023 waziri mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa alipiga marufuku matumizi ya madumu yanayotumika kupima mafuta ya mawese maarufu kwa jina la bidoo lakini bado baadhi ya wafanyabiashara wanaendelea kuyatumia.