Joy FM

Ndoto za watoto zinalindwa na kuendelezwa?

10 November 2026, 12:35

Ni baadhi ya wananchi wakiwa katika semina, Picha na Prisca Kizeba

Watoto ni zawadi na hazina kubwa katika jamii kwa sababu wao ndio viongozi wa kesho na kila mtoto ana ndoto na matarajio yake kuhusu maisha ya baadaye wapo watoto wanaotamani kuwa madaktari, walimu, marubani, marais, wahandisi, wanamichezo na wataalamu wengine mbalimbali hivyo basi, ni wajibu wa wazazi, walimu, viongozi na jamii kwa ujumla kulinda na kuendeleza ndoto za watoto ili waweze kutimiza malengo yao

Na Prisca Kizeba

Uongozi wa shirika la Compasion Mwasenga umewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanalinda ndoto za watoto wao  kwa kuweka msingi imara ya madili, nidhamu, mawasiliano na uangalizi wa karibu

Hayo yameelezwa na Afsa wa ulinzi wa mtoto ambaye pia ni Mratibu wa kituo cha Compation kilichopo Mwasenaga Manispaa ya Kigoma Ujiji Bw. Robart Petro wakati akitoa Semina kwa wazazi na Walenzi   katika kituo hicho.

Amesema wazazi na walezi wana wajibu wa kuweka mawasiliano mazuri na mtoto wao kwa kuwasikiliza kuwajengea  uwezo   wa kujiamini.

Semina ikiendelea kwa wazazi na walezi, Picha na Prisca Kizeba

Naye Mwenyekiti Mstaafu wa Makanisa ya Kipetekost (CPCT)  Mchungaji Augustino Jafari Kizeba ambaye pia Mlenzi wa watoto katika kituo hicho amsema kila dhehebu au dini linawajibu wa kuoa elimu kuhusu ulinzi wa mtoto ili  kuendelea kutegeneza kizazi chenye maadali mema.

Baadhi ya wazazi waliohidhuria semina hiyo wasema kuwa mzazi anatakiwa kuwa kio cha kutengeza mustabali mzima wa malezi ya mtoto wake bila kujali anapungufu gani.

Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa kwenye semina, Picha na Prisca Kizeba