Joy FM

Siku 16 za kupinga ukatili zazinduliwa Kigoma

25 November 2026, 12:18

Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Picha na Josephine Kiravu

Jukumu la kutokomeza ukatili si la mamlaka pekee, bali linahitaji ushiriki wa kila mwanajamii ili kujenga mazingira salama yenye haki na usawa

Na Josephine Kiravu

Jamii Mkoani Kigoma imetakiwa kuondokana na mfume dume ambao umekuwa kandamizi na badala yake kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi pindi linapotokea tukio la ukatili kwa watoto.

Hayo yamejiri wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto mkoani Kigoma ambapo Mkuu wa polisi jamii ACP Juma Majura amesema wamefanikiwa kupunguza makosa ya ukatili kutoka makosa 1050 kwa mwaka 2025 hadi 608 kwa mwaka 2026.

Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Picha na Josephine Kiravu

Amesema miongonu mwa makosa ambayo yamekuwa yakiripotiwa kwa kiasi kikubwa ni yale ya ukatili wa kingono pamoja na utelekezaji watoto unaotokana na ndoa nyingi kudai talaka mahakamani na watoto kukosa uangalizi wa wazazi wote wawili.

Akizungumza  kwa niaba ya Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa Katibu tawala msaidizi Bi. Zabibu Mkamba ameitaka jamii kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika ili kuondoa kabisa ukatili kwa wanawake na watoto.

Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Picha na Josephine Kiravu

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa  kijinsia kwa mwaka huu 2026 yamebebwa na kauli mbiu  isemayo Tuungane kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto Jenga Taifa imara lenye haki na usawa kuelekea Dira 2050.