Storm FM

Amnyonga hadi kufa mtoto wa boss wake Geita

28 October 2026, 9:34 am

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Kale Chongela

Chanzo cha tukio hilo kinahusishwa na imani za kishirikina baada ya dada huyo wa kazi kupandisha mapepo kisha kumnyonga mtoto huyo ndani ya nyumba.

Na: Kale Chongela

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Mfanyakazi wa ndani aliyetambulika kwa jina la Verediana Levee  kwa tuhuma za kumuua mtoto Wiliamu Mathayo mwenye umri wa miaka 5 kwa kumnyonga shingo.

Baba mzazi wa marehemu Bw Mathayo Valence Akizungumza na Storm Fm amesema tukio hilo limetokea yeye akiwa katika majukumu yake  ambapo wakati akitoka nyumba mfanyakazi huyo alimuacha na watoto wengine na fedha za matumiza na watoto wakiwa wazima katika hali ya kushangaza ndipo alipewa taarifa kuwa mtoto wake amafariki kwa kunyongwa na mfanya kazi wake.

Sauti ya baba mzazi wa marehemu

Nyumba ambayo wanaishi familia ya marehemu mtoto huyo na tukio lilipotokea.Picha na Kale Chongela

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ibolelo Bw Juma Ramadhani Luge ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi katika mtaa huo kufahamu historia ya mfanya kazi kabla ya kumpa kazi ili kuepukana na changamoto zinazoweza kuleta madhara .

Sauti ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ibolelo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Safia Jongo amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusemakuwa tukio hilo limetokea oktoba 24 majira ya saa nne  katikia mtaa wa Ibolelo maarufu kwa jina la mwabasabi kata ya Nyankumbu manispaa ya Geita huku akitaja chanzo cha tukio hilo ni Imani za kishirikiana.

Sauti ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita