Storm FM

Aliyeomba Mungu ajifungue pacha ajifungua wanne

10 July 2024, 10:58 am

Watoto wanne waliozaliwa katika hopitali ya halmashauri ya mji Geita. Picha na Edga Rwenduru

Baada ya kumuomba Mungu amjalie watoto pacha, hali imekuwa tofauti baada ya kujaliwa watoto wanne wote wakiwa wa kike.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Elizabeth Vicent (30) mkazi kata ya Nyankumbu, halmashauri ya mji wa Geita amejifungua watoto wanne baada ya maombi yake ya muda wa zaidi ya miaka mitano akiomba ajifungue watoto pacha.

Mwanamke huyo amejifungua mapacha hao Julai 3, 2024 kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Geita ambapo mpaka sasa watoto hao wapo chini ya uangalizi wa madaktari kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati (njiti).

Elizabeth Vicent akiwa na watoto wake baada ya kujifungua. Picha na Edga Rwenduru

Wakati akizungumza na waandishi wa Habari Elizabeth amesema baada ya kujifungua mtoto wake wa tatu alikaa kwa muda wa miaka mitano bila kupata ujauzito ndipo alipoamua kufanya maombi ili apate ujauzito tena.

Sauti ya Elizabeth Vicent

Rafiki wa mume wa mama huyo Mafunda Ligasa ameeleza kwa furaha baada ya taarifa ya kupokea watoto hao.

Sauti ya shemeji

Mganga mfawidhi wa hospitali ya mji wa Geita Dkt. Thomas Mafuru amezungumza kitaalamu namna bora ya kuwatunza watoto hao.

Sauti ya Dkt. Thomas Mafuru
Mganga mfawidhi wa hospitali ya halamshauri ya mji Geita. Picha na Edga Rwenduru