Storm FM

Geita wafanya dua maalum ya Hayati Mwinyi

3 March 2024, 4:40 pm

Waumini wa msikiti wa Ijumaa Geita wakiwa katika dua ya kumuombea Hayati Mwinyi. Picha na Mrisho Sadick

Mamilioni ya watanzania wameendelea kumuombea dua Hayati Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na Mrisho Sadick:

Waumini wa dini ya kiislamu wa Msikiti wa Ijumaa Halmashuri ya mji wa Geita Mkoani Geita wamefanya ibada maalum ya kumuombea heri kwa mwenyezi Mungu Hayati Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shekhe wa Mkoa wa Geita Al Haji Yusuph Kabaju amewaongoza waumini wa dini hiyo , wananchi na viongozi wa serikali na vyama vya siasa Mkoani Geita kumuombea Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Ali Hassan Mwinyi pamoja na viongozi mbalimbali wa dini hiyo waliyo hai na waliyotangulia mbele za haki.

Sauti ya Shekhe wa Mkoa wa Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameshiriki katika ibada hiyo amezungumza kwa niaba ya serikali na wananchi wa Mkoa wa Geita ambapo amesema serikali itaendelea kutambua nakuthamini mchango wa viongozi wa dini.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi Mkoani Geita kuendelea kulinda nakuitunza amani ya nchi.

Sauti ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita