Storm FM

GGML yafanya makubwa maonesho ya 6 ya madini

29 September 2023, 9:15 pm

Wafanyakazi wa GGML katika maonesho ya 6 ya kimataifa ya madini Geita

Geita Gold Mine Limited umeendelea kuwa mgodi wa mfano katika masuala ya teknolojia ya madini na elimu kwa wananchi.

Na Zubeda Handrish- Geita

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa kiasi cha Sh. milioni 150 kudhamini Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kila mwaka, yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili, kata ya Buhalahala mkoani Geita.

Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na Mawasiliano GGML Stephen Mhando wakati waziri wa madini Anthony Mavunde akipita katika banda la maonesho la mgodi huo huku akiongeza kuwa kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Geita kujenga uwanja

Sauti ya Meneja Uhusiano na Mawasiliano GGML Stephen Mhando

Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka, mwaka huu yanatarajiwa kuzinduliwa tarehe 23 na kuhitimishwa tarehe 30 Septemba.

Maonyesho hayo yanafanyika kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), katika viwanja vya Bombambili vilivyopo eneo la Mamlaka ya Maeneo ya Usindikaji Nje (EPZA) mkoani humo.

Akizungumzia ushiriki wa GGML katika maonesho hayo, Meneja Mwandamizi wa kampuni hiyo anayesimamia mahusiano jamii, Gilbert Mworia alisema maonesho hayo yamekuwa na mvuto wa kipekee tangu yalipoasisiwa kutokana na ufadhili wa GGML kupitia mfuko wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) ambao uliwezesha ujenzi wa eneo hilo la EPZA pamoja na eneo la uwanja huo wa maonesho.