Storm FM

Mke achukuliwa vitu vya ndani bila ya mume kujua, akidaiwa mkopo

6 September 2023, 11:46 am

Tukio la sofa na sabufa vilivyochukuliwa na kampuni ya mikopo ya Gold

Matukio ya watu waliochukua mikopo katika makampuni ya kukopesha fedha na kushindwa kurejesha fedha hizo yamekithiri, huku tukio la mke kukopa bila ya kumshirikisha mume na kushindwa kurejesha na kuchukuliwa vitu vya ndani limeacha watu vinywa wazi.

Na Zubeda Handrish- Geita

Kufuatia tukio la Mwanamke mmoja anaefahamika kwa jina la Winiesta Achiem, mkazi wa mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu, wilayani na mkoani Geita la kusombewa vitu vya ndani (sofa na sabufa) na kampuni ya kukopesha fedha ya Gold iliyopo mtaani hapo baada ya kukopa bila ya kumwambia mumewe na kushinda kurejesha, Mume wa mwanamke huyo Bw. Janes Fabian ambaye mpaka tukio hilo linatokea hakuwa anajua amezungumzia juu ya sakata hilo.

Sauti ya Bw. Janes Fabian, mume wa Winiesta Achiem
Sauti ya Bw. Janes Fabian, mume wa Winiesta Achiem

Nae Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Enos Cherehani amezungumza namna alivyopokea taarifa ya tukio hilo katika mtaa wake na hatua alizochukua baada ya kupokea malalamiko ya vitu vya mwananchi wake vya ndani kuchukuliwa na kampuni ya mikopo bila ya ridhaa ya baba wa familia.

Sauti ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Uwanja Bw. Enos Cherehani

Kampuni hiyo inayofahamika kwa jina la Gold, bado tunaendelea kufanya ufuatiliaji ili kujua hasa juu ya tukio hilo, kwani juhudi ziligonga mwamba baada ya kukuta ofisi hiyo imefungwa na namba za simu za viongozi zikiwa hazipatikani.

Afisa Biashara wa halmashauri ya mji wa Geita Sulemani Said Mawalanga amezungumzia tukio hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa huo wa Uwanja, huku akiahidi kufanya ufuatiliaji kwa makampuni hayo ya kukopesha fedha yanayofanya shughuli zake kinyume cha taratibu.

Sauti ya Afisa Biashara wa halmashauri ya mji wa Geita Sulemani Said Mawalanga.