Storm FM

Mufti wa Tanzania abariki ujenzi wa msikiti Geita

6 April 2024, 4:22 pm

Mufti wa Tanzania akiweka jiwe la msingi msikiti wa Ijumaa Geita . Picha na Mrisho Sadick

Mwezi mtukufu wa ramadhani umekuwa na manufaa makubwa kwa waumini wa dini ya kiislamu Mkoa wa Geita baada ya kiongozi wao mkuu kuwatembelea nakubariki ujenzi wa msikiti.

Na Mrisho Sadick – Geita

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir ametembelea nakuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa msikiti Mkuu wa Mkoa wa Geita huku akiwataka waumini wa dini hiyo kujitoa kwa hali na mali ili kukamilisha ujenzi huo.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa msikiti huo mbele ya mufti wa Tanzania katibu wa BAKWATA Mkoa wa Geita Abbas Mtunguja amesema wanajenga msikiti wa ghorofa tatu nakwamba wamekwama kuendelea na ujenzi huo ghorofa ya kwanza na pili kutokana na ukata wa fedha.

Mufti wa Tanzania akiwa na viongozi wa msikiti wa Ijumaa Geita. Picha na Mrisho na Sadick
Sauti ya katibu wa BAKWATA

 Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewapongeza waumini wa dini Mkoani Geita kwa kuanzisha ujenzi mkubwa wa msikiti huo nakuwataka kuendelea kujitoa zaidi ili kukamilisha ujenzi huo wakati akiendelea kutafuta wadau wa kuwaunga mkono.

Sauti ya Mufti wa Tanzania
Waumini wa msikiti wa Ijumaa mjini Geita. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya waumini wa dini hiyo Mkoani Geita wamempongeza Mufti wa Tanzania kwa kutembelea nakuweka jiwe la msingi kwenye msikiti huo nakuahidi kuendelea kujitoa ili kufikia malengo yao.