Storm FM

Geita mji yapewa siku 30 kukamilisha Zahanati zote zilizotelekezwa

16 November 2023, 12:34 pm

Mkuu wa Mkoa wa Geita mwenye kofia nyeusi na miwani akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Geita katika ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa Zahanati. Picha na Evance Mlyakado

Kutelekezwa kwa Zahanati zaidi ya tatu katika Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita kumemuibua Mkuu wa Mkoa nakutoa maagizo kwa watendaji wa serikali katika eneo hilo.

Na Mrisho Sadick – Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ametoa mwezi mmoja kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita kuhakikisha anakamilisha Zahanati zote zilizotelekezwa kwa muda mrefu katika halmashauri hiyo.

Shigela akiwa katika ukaguzi wa miradi hiyo ametembelea ujenzi wa zahanati ya Bombambili, Mwatulole na Bwihugule ambazo zimetelekezwa kwa muda mrefu nakuiagiza halmashauri ya mji wa Geita kuhakikisha zinakamilisha ujenzi huo haraka ili wananchi waanze kupata huduma karibu na makazi yao.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita Zahra Michuzi ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa muda waliyopewa nakwamba kufiki tarehe 15 mwezi wa kwanza mwaka kesho Zahanati hizo zitakuwa zimekamilika huku meneja Mwandamizi anayeshughuliki mahusiano ya jamii kutoka GGML Gilbert Mworia akisema watashirikiana na halmashauri ya mji kutekeleza agizo hilo.

Sauti ya Mkurugenzi Geita mji na Mwakilishi wa GGML
Moja ya Zahanati iliyotelekezwa kwa muda mrefu katika Mtaa wa Mwatulole Geita mjini. Picha na Evance Mlyakado

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amemuahidi mkuu wa mkoa wa Geita kuwa atasimamia utekelezaji wa miradi hiyo kila hatua ili ikamilike kwa muda uliyopangwa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Geita