Storm FM

DC Geita aagiza GEUWASA kukamilisha mradi wa maji Nyankanga

3 June 2024, 4:24 pm

Mkuu wa wilaya ya Geita (kulia) akiteta na meneja ufundi kutoka GEUWASA Isack Mgeni (kushoto) . Picha na Kale Chongela

Licha ya matarajio ya kukamilika wa mradi mkubwa wa maji maarufu kwa Bwawa la Nyanakanga ili kuweza kuwasaidia wananchi, bado hali ni tete kutokana na mkandarasi kusua sua katika utekelezaji wa mradi huo.

Na: Kale Chongela – Geita

Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashimu A Komba ameiagiza mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita GEUWASA kukamilisha mradi wa maji wa Nyankanga kabla ya julai 2024 maagizo aliyoyatoa baada ya kufanya ziara katika eneo la utekelezaji wa mradi huo.

Sauti ya DC Geita
Muonekano wa mradi wa maji Nyakanga. Picha na Kale Chongela

Meneja wa usambazaji maji kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita GEUWASA mhandisi Isack Mgeni akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya DC Komba amesema wamelazimika kuvunja mkataba na mkandarasi GIPCO company limited kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo kinyume na makubaliano.

Sauti ya meneja ufundi wa GEUWASA
Muonekano wa mradi wa maji Nyakanga. Picha na Kale Chongela

Mradi huo wa maji wa Nyankanga unajengwakwa thamani ya kiasi cha shilingi bilioni 1.1.