Zaidi ya watoto 55,000 kupatiwa chanjo mjini Geita
6 June 2024, 9:57 am
Serikali imeendelea kuimarisha utoaji chanjo kwa makundi mbalimbali ya watu katika jamii ikiwemo watoto chini ya umri wa miaka mitano ili kuwakinga na maradhi mbalimbali.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Watoto zaidi ya 55,000 wenye umri chini ya miaka 5 katika halmashauri ya mji wa Geita wanatarajiwa kupatiwa matone ya vitamin A na dawa za minyoo kwa kipindi cha mwezi juni mwaka huu.
Akizungumza katika kampeni ya utoaji wa matone ya vitamin A na dawa za minyoo kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5 Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Geita Dkt. Sunday Mwakyusa amesema licha ya malengo waliyojiwekea bado wanakumbwa na changamoto ya mapokeo hasi kutoka kwa wazazi na walezi juu Imani zao kuhusu chanjo
Aidha kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Geita Lucy Beda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeini hiyo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Geita ametoa rai kwa akina mama kuzingatia lishe kwa watoto wao.
Nao baadhi ya akina mama waliojitokeza katika uzinduzi huo wameshukuru kupatiwa elimu ya lishe na wataalamu wa Afya.