Storm FM

Shirika la Plan International lawafuta machozi wasichana

26 April 2024, 11:47 am

Baadhi ya baiskeli ambazo zimetolewa kwa wanafunzi wa kike mkoani Geita ili kukabiliana na changamoto ya umbali. Picha na Kale Chongela

Mradi wa KAGIS (Keeping Adolescent girls in shool) ambao unaratibiwa na shirika la Plan international umeendelea kuacha alama kwenye sekta ya elimu mkoani Geita kwa kuendelea kupunguza changamoto zinazowakabili watoto wa kike kuendelea na masomo.

Na Kale Chongela – Geita

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela amepiga marufuku tabia ya baadhi ya wazazi na walezi mkoani Geita kutumia baiskeli ambazo zinatolewa kwaajili ya wanafunzi wa kike kwenda shuleni kutokana na changamoto ya umbali.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza katika hafla ya ugawaji baiskeli kwa watoto wa kike. Picha na Kale Chongela

Na: Kale Chongela – Geita

Ameeleza hayo katika hafla ya ugawaji wa baiskeli zaidi ya 500 zenye thamani ya shilingi milioni 180 ambazo zimetolewa na shirika la Plan International mkoa wa Geita kupitia mradi wa KAGIS (Keeping Adolescent Girls in School) wenye lengo la kuondoa changamoto mbalimbali za kielimu zinazowakabili watoto wa kike.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Geita
Mkurugenzi wa miradi wa Plan internation Bw. Laurent Wambura katika hafla ya ugawaji baiskeli kwa watoto wa kike. Picha na Kale Chongela

Mkurugenzi wa miradi wa shirika hilo Bw. Laurent Wambura amesema lengo la kutoa baiskeli hizo ni kuwasaidia watoto wa kike kutimiza ndoto zao na kuondoa vikwazo vinavyopelekea washindwe kwenda shule kutokana na umbali.

Sauti ya mkurugenzi wa miradi

Baadhi ya wasichana ambao wamepewa baiskeli hizo wameshukuru kwa hatua hiyo na kuahidi kuwa zitawasaidia kuweza kufika shuleni kwa kuepuka vishawishi na kuondoa changamoto ya utoro

Baadhi ya watoto wa kike na wazazi waliohudhuria katika hafla ya ugawaji wa baiskeli. Picha na Kale Chongela
Sauti ya baadhi ya wanafunzi waliopewa baiskeli