Storm FM

Wahitimu vyuo vya Biblia watakiwa kuisaidia jamii

10 July 2023, 3:35 pm

Wahitimu wa Chuo cha Biblia Uyovu wakiwa kwenye Mahafali. Picha na Kale Chongela

Wahitimu wa vyuo mbalimbali vya Biblia wa Muungano wa makanisa ya Kipentekoste Tanzania wametakiwa kutumia ujuzi na elimu ambayo wanaipata kwenye vyuo hivyo kuisaidia jamii.

Na Kale Chongela:

Askofu Mkuu wa makanisa ya kipentekoste Tanzania Eliaza Issack  amewataka wahitimu wa vyuo vya Biblia kutumia elimu yao katika kukemea ushoga na kufundisha watu kuifuata njia ya kweli katika imani.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waumini wa kanisa la ( MMPT ) katika kanisa la Pentkoste lililopo mamlaka ya mji mdogo wa Katoro alipokuwa akiwahusia wanafunzi ambao wamehitimu chuo  cha biblia uyovu tawi la Katoro.

Askofu Mkuu wa Muungano wa Makanisa ya Kipentekoste MMPT Eliaza Issack. Picha na Kale Chongela
Sauti ya Askofu Mkuu Eliaza Issack

Kwa  upande wao  baadhi ya wahitimu wa chuo cha biblia wameahidi kuwa tayari kuitumikia jamii kwa kuhubiri habari njema  kwa kuzingatia maandiko ya vitabu vitakatifu.  

Sauti za wahitimu wa chuo cha Biblia Uyovu

Aidha  Mkurugenzi wa Chuo cha Biblia  Mchungaji Elifazi John amesema wahitimu kwa ngazi ya Astashahada  ni 13 kati ya hao mwanamke ni mmoja na ngazi ya Cheti 17.